Kanuni za jukwaa la AlphaNow kwa wenyeji na wasaidizi.
Nita…
Tengeneza mazingira yatakayofanya washiriki wahisi kukubalika na kuheshimiwa
Dumisha viwango vya siri tulivyokubaliana kabla, wakati wa kozi na baada ya kozi ya Alpha
Hakikisha kuwa wageni kamwe hawatakua kwenye ‘chumba’ cha mtandao bila mwenyeji au msaidizi
Ripoti haraka iwezekanavyo ukiukaji wowote wa kanuni hizi kwa kiongozi wa kanisa langu, kiongozi wa Alpha au msimamizi ili kuwalinda wanyonge
Sita…
Ruhusu kozi yangu ya Alpha kurekodiwa
Bagua mtu yoyote au kutukana, au kutumia lugha ya kibaguzi, au inayohusiana na ngono au ya kuleta dharau
Weza kuvumilia matusi, ubaguzi, maneno yanayochochea ngono au lugha ya dharau kutoka kwa watu wengine
Tengeneza, kutafuta, kusambaza au kutuma picha za ngono au itikadi za kikaidi kwa kutumia jukwaa la AlphaNow, na pia sitatuma ujumbe wowote unaohusiana na ngono